
Orgasmic dysfunction ni hali ya ya kutofika kileleni wakati wa tendo la ndoa. Hali hii inaweza kutokea hata kama mwanamke ameandaliwa vizuri na hisia zake zimeamshwa kufanya mapenzi. Hali hii ya kutofika kileleni inaweza kutokea kwa watu wote mwanamke na wanamume, japo inawapata zaidi wanawake. Kufika kileleni (orgasm) ni kiwango cha juu cha hisia ambazo mtu anapata pale anapofanya tendo la ndoa. Mguso wa hisia wakati wa kufanya mapenzi hufanya mwili kutoa kemikali ambazo zinakufanya ujiskie raha ya hali ya huu zaidi pale unapokuwa kitandani na mwenzi wako. Wanawake wengi sana hawajawahi kufika kileleni na kuonja raha ya kufanya tendo la ndoa, japo wengine wamepata na watoto, lakini bado hawajawahi kuona raha ya kufikia mshindo. Nimekuwa nikipokea kesi nyingi za wakina mama kwa tatizo la kutofika kileleni na ndio maana nimeleta makala hii iwe msaada kwako, endelea kusoma
Nini Kinasababisha Mwanamke Kutofika Kileleni kwenye Tendo la ndoa?

- Umri mkubwa
- Magonjwa kama kisukari
- Mgonjwa kuwa na historia ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi
- Matumizi ya vidonge kwa ajili ya sonona
- Imani za kidini au kikabila
- Woga wakati wa kufanya mapenzi
- Kuhisi kama mwenye makosa kwenye kufanya mapenzi
- Historia ya kunyanyaswa kingono mfano kubakwa
- Msongo wa mawazo
- Kushindwa kutambua thamani yako mfano kuhisi kama huna thamani mbele ya mwenzi wako na jamii kwa ujumla
- Matatizo kwenye mahusiano na
- Kuvurugika kwa homoni
Kushindwa kufika kileleni kunagawanyika katika makundi ma4
- Primary anorgasmia: Hali ya kutowahi kabisa kufika kileleni hata mara moja
- Secondary anorgasmia: Kushindwa kufika kileleni japo siku za nyuma uliwahi kufurahia
- Situational anorgasmia: Hali ya kufika kilelni kwenye matukio flani flani tu, mfano ukifanya ngono kupitia mdomo(oral sex) ama ukipiga punyeto.
- General anorgasmia: Ni hali ya kutofika kileleni kwenye mwzingira ypyote yale, hata kama utaandaliwa vizuri na kupata msisimuko wa kihisia.
Matibabu kwa Mwanamke Kushindwa Kufika Kileleni
Matibabu ya tatizo hili yanatofautiana kwa kulingana na chanzo chake. Tiba hizi zinaweza kujumuisha- Kuacha matumizi ya dawa
- Kupata ushauri wa kisaikologia
- Mwanamke kuandaliwa vizuri kabla ya kufanya mapenzi
Watu wanalichukuliaje tatizo hili la Mwanamke kushindwa kufika Kileleni
Mwanamke kushindwa kufika kileleni inaweza kuwa ni tatizo la kuleta mawazo na hata kutishia kuvunjika kwa mahusiano. Wanaume wengi huwalaumu wake zao kwamba wana michepuko ndio maana hawatosheki . Kama wewe ni mwanamke ambaye unapitia tatizo hili tambua kwamba haupo peke ako. na pia fahamu kwamba inawezekana kutibu tatizo hili na ukafurahia tendo la ndoa. Cha muhimu ni kufahamu tu chanzo cha tatizo lako. Unaweza kufika hospitali ukaonana na Daktari wako akakupa mwongozo jinsi ya kupata tiba.
Tags
Elimu ya mahaba