Jambazi aliye toroka jela kwa kutumia helkopter akamatwa ufaransa

Admin
By -
0
Redoine Faid, jambazi sugu raia wa Ufaransa ambaye alitoroka jela akitumia helikopta iliyokuwa imetekwa nyara amekamatwa tena na polisi.
Mhalifu huyo aliyekuwa akisakwa na vyombo vya ulinzi nchini Ufaransa, alishikwa kaskazini mwa jiji la Paris, akiwa na ndugu yake na watu wengine wawili kwa mujibu wa ripoti ya polisi.
Faid, 46, amenukuliwa awali akisema kuwa yeye ni shabiki wa filamu za uhalifu, ambazo anadai zimemfundisha jinsi ya kufanya uvamizi.
Mwaka 1998 alikamatwa kwa mara ya kwanza kwa shitaka la wizi wa kutumia mabavu. Tukio la kutoroka jela mwezi wa julai mwaka huu ni la pili kwa mhalifu huyo.
Alitoroshwa kutoka gereza moja huko Reau, kusini mashariki mwa Paris, na watu watatu waliokuwa wamejihami vikali. Kisha wakamuingiza kwenye ndege aina ya helikopta iliyoendeshwa na rubani aliyekuwa ametekwa nyara.

Redoine Faid alikamatwa mji wa nyumbani kwake huko CreilHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRedoine Faid alikamatwa mji wa nyumbani kwake huko Creil

Kukamatwa kwake kunakuja saa kadhaa baada ya waziri wa mambo ya ndani Gérard Collomb kujiuzulu katika pigo jipya kwa ya Rais Emmanuel Macron.
Wizara hiyo ya mambo ya ndani itaongozwa kwa muda na waziri mkuu Édouard Philippe.

Redoine Faid ni nani?

Jamabazi huyo anadai kuwa filamu za Hollywood, kama vile filamu maarufu ya uhalifu ya Scarface iliyoigizwa na nyota Al Pacino, ilichangia mfumo wa maisha yake.
Wakati mmoja alienda kwa mtengeza filamu hiyo Michael Mann kwenye tamasha ya filamu la Paris na kamwambia: "Wewe ulikuwa mshauri wangu wa kiufundi."

This file photo taken on 15 April 2013 in Paris, a screenshot of the Interpol website, shows the international wanted person notice for French robber Redoine Faid.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRedoine Faid aliorodheshwa na Interpol mwaka 2013

Mwaka 2013 alitoroka jela mara tu baada ya kuwasili akitumia vilipuzi kulipua milango mitano ya gereza huku akiwashika walinzi mateka na kuwatumia kama ngao.
Umaarufu wake umechangiwa na kitabu chake cha mwaka 2009, kinachosimulia maisha yake toka akiwa mdogo kwenye mitaa ya Paris mpaka kuwa mhalifu sugu.

Maisha ya Redoine Faid

  • Maisha ya Faid ya kufungwa jela na kutoroka yalianza mwaka 1998 kutokana na makosa ya wizi wa kutumia nguvu na kupora benki.
  • Mwaka 2009 aliachiliwa kwa msamaha akiapa kuwa alikuwa amebadilika lakini ilipofika mwaka 2011 alikuwa amekiuka makubaliano ya kuachiliwa kwake na akarudishwa korokoroni.
  • Mwaka 2017 Faid alihukumiwa miaka 10 baada ya kutoroka jela ya Séquedin, mwaka 2013 nje ya mji wa Lille. Pia alihukumiwa miaka 18 kwa kupanga wizi mwaka 2010 ambapo polisi mmoja Aurélie Fouquet, aliuawa.
  • Faid alishindwa katika rufaa aliyoikata na Aprili mwaka 2018 alihukumiwa kifungo zaidi cha miaka 25 kwa wizi. Alikuwa akitumikia kifungo hicho wakati wa kisa cha hivi majuzi cha kutoroka jela
  • Alizaliwa mwaka 1972 na kukulia maeneo yenye visa vya uhalifu mjini Paris.
  • Miaka ya 1990 aliongoza genge lilohusika kwenye wizi na kupora watu mjini Paris.
  • Mmoja wa wasimamizi wa hivi punde wa Faid gerezani alisema - hakuwa na mzozo wowote na walinzi lakini tulikuwa na hofu kila wakati.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)