Dar es Salaam.Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimepokea barua mbili za malalamiko kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi wa Kinondoni kikidaiwa kuvunja kanuni za maadili ya uchaguzi.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila amewaambia wana habari leo Jumatano Februari Mosi 2017 kuwa barua wamezipokea jana kutoka kwa Mkurugenzi wa Kinondoni Aron Kagurumjuli.
Amesema barua ya kwanza inaeleza kuwa Chadema inadaiwa kufanya kampeni nyumba kwa nyumba Januari 28 katika eneo la Kigogo Mbuyuni hadi Londor Bar badala ya siku kuwa Kata ya Ndugumbi kama ratiba inavyoonyesha.
Kigaila amesema barua ya pili ni malalamiko kutoka kwa chama CUF kilichodai Chadema kinatumia salamu ya chama chao katika majukwaa ya kampeni, kinaweka bendera CUF katika majukwaa yao.
"Madai mengine ni kwamba viongozi wa CUF wana kuja katika mikutano yetu na kukaa meza kuu na kupanda katika majukwaa.
Alisema kwamba yeye hajatoa barua kwa Chadema pekee ametoa barua kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi mdogo Kinondoni, hivyo kinachotakiwa ni kutia majibu na kufuata taratibu
“Mimi nashangaa wanakimbilia kwenye vyombo vya habari wakati barua hawajapatiwa peke yao wanachotakiwa ni kufuata taratibu za kampeni na si vinginevyo’’alisema
Tags
Siasa