SIMBA WAAMUA KUJA KIVINGINE

Kocha mpya wa Simba SC aja kivingine kuivaa Majimaji leo. Kikosi cha Simba kimetoka kikielekeza mfumo wa4-1-2-3 . Hii ina maana Simba watatumia ‘ diamond midfield ‘ ikiwa chini ya Jonasi Mkude chini na juu yake wakisimama Shiza Kichuya kushoto , kulia Jamali Mwambeleko huku Saidi Ndemla akifunga juu ambaye ndie atakuwa playmaker kwenye kiungo kuleta muunganiko na washambuliaji wawili wa juu kwa njia ya kati Emanuel Okwi na John Rafael Bocco.

Nyuma kutakuwa na walinzi wanne ; Asante kwasi kulia na Shomari Kapombe kulia huku Juuko Murshid na Erasto Nyoni wakisimama kati kumlinda Aishi Manula langoni huku juu wakilindwa na Jonasi Mkude.

Ni mfumo ambao una variations nyingi kulingana na approach ya mwalimu , uwezo wa wachezaji na nguvu ya mpinzani wako.

Endapo Majimaji watakuwa na kiungo kizuri kuipa tabu Simba eneo la kati ambalo mara nyingi kwenye diamond midfield hutengeneza mashimo endapo deep lying holding midfielder atacheza sana chini ( kwa hapa Mkude ) , Simba itawalazimu kubadilika aidha kucheza 3-4-3 ili kujaza watu kati , pia wanaweza kurudi katika mfumo wao wa 3-5-2 ili kuziba mashimo , kumiliki mpira na kujenga ngome kali kati itakayoendeswa kwa pasi fupi fupi za kasi kikubwa Link ya Mkude, Ndemla na Emanuel Okwi iwe imara kuijenda central line kwenye ‘ direct ‘ play.

Lakini pia uwepo wa Ndemla na Emanuel Okwi unaweza kuwafanya Simba kucheza 4-3-3 ambayo huhitaji viungo washambuliaji wawili wenye uwezo mzuri wa kuchezesha timu na kupiga toka mbali kama deception plan kwa maana mmoja husimama kama invisible midfielder kwa maana ya kucheza sana chini kama kiungo mchezeshaji.

Tusubiri dakika 90 kuona mfaransa anatupa kitu gani katika mfumo wake huu mpya ingawa si badiliko kubwa ambalo litawafanya Simba kuanza upya kwa sababu kiufundi ni mfumo ambao bado una msingi ule ule wa Simba kutumia wide formations ambazo zinahitaji viungo kuamua mechi.

KIKOSI CHA SIMBA SC VS MAJIMAJI

1-Aishi Manula
2-Shomary Kapombe
3-Asante Kwasi
4-Juuko Murshid
5-Erasto Nyoni
6-Jonas Mkude
7-Shiza Kichuya
8-Said Ndemla
9-John Bocco
10-Emmanuel Okwi
11-Jamal Mwambeleko

Akiba
-Emmanuel Mseja
-Hussein Mohamed
-Nicholas Gyan
-Mwinyi Kazimoto
-James Kotei
-Mzamiru Yassin
-Laudit Mavugo


Post a Comment

Previous Post Next Post