NDONDO CUP YAMPA TUZO MTOTO NA KUMSOMESHA MPAKA CHUO

Usiku wa Agosti 21, 2017 Mohamed Rashidi maarufu kwa jina la ‘kitoto cha Ndondo’ alitangazwa mshindi wa tuzo ya shabiki bora (bila kushindania) wa mashindano ya Ndondo Cup 2017.



Kitoto cha Ndondo alikuwa anahudhuria mechi zote za mashindano huku akiwa katika mwonekano tofauti, mara zote alikuwa akiambatana na baba yake mzazi Bw. Rashidi.



Mwonekano wake uliiongezea ladha Ndondo Cup na kuifanya kuwa na mwonekano wa kipee, kwa kuzingatia hilo waratibu wa mashindano waliamua kumpa shavu dogo huyo kwa kumsomesha kuanzia elimu ya awali hadi atakapoishia.



Imepita miezi kadhaa tangua ahadi hiyo ilipotolewa huenda baadhi ya wadau walidhani mpango huo umekufa, leo Januari 22, 2018 ahadi hiyo imetekelezwa. Dogo amelipiwa ada ya shule katika shule ya Tussime iliyopo maeneo ya Tabata.



Tayari amekabidhiwa kwa uongozi wa shule (Tusiime) na mara moja ameanza masomo yake ya ngazi ya awali katika shule hiyo.



Tunaamini umahiri wake aliouonesha kwenye Ndondo atauhamishia darasani na kufanya makubwa zaidi.



Ndondo Cup inamtakia kila la heri Mohamed ‘kitoto cha Ndondo’ katika kipindi chake chote cha masomo lakini tutaendelea kukutana nae kwenye viwanja vyetu vya Ndondo.


Post a Comment

Previous Post Next Post