
Utafiti hou uliofanywa kwa zaidi ya vijana 2000 nchini India ulionyesha kuwa wengi waliokuwa na ugonjwa wa moyo walikuwa na upara na nywele za kijivu ikilinganishwa na wanaume walio na nywele kichwani.
Utafiti huo wa Idara ya magonjwa ya moyo barani Ulaya unatarajira kusoomwa katika kongamano la kila mwaka la magonjwa ya moyo nchini India.
Lakini wakfu wa Uingereza unaosimamia magonjwa ya moyo umesema kuwa sababu nyengine hatari pia ni muhimu.
Daktari Mike Knapton, amesema kuwa utafiti huo miongoni mwa wanaume wenye upara na nywele za kijivu unaweza kuwagundua wale walio na hatari ya matatizo ya magonjwa ya moyo.
Hata hivyo hilo sio jambo ambalo linaweza kubadilishwa na watu, wakati ambapo unaweza kudhibiti hali ya maisha mbali na sababu zinzoweza kuhatarisha maisha kama vile viwango vya juu vya mafuta na shinikizo la damu.Hivi ni vitu muhimu zaidi kufuatilia
Tags
afya