WATANZANIA 23.WAKAMATWA NCHINI KENYA

Leo December 29, 2017 nikusogezee stori kutoka nchini Kenya kwa Uhuru Kenyatta ni kuhusiana na Watanzania ishirini na tatu wamekamatwa  katika eneo Malindi, kata ya Kilifi kwa kudaiwa kushiriki katika shughuli za uvuvi kinyume cha sheria katika Bahari ya Hindi upande wa Kenya.

Kwa mujibu wa kituo cha Television ya CITZENTV, msaidizi wa Kamanda wa Polisi Jimbo la Kilifi, Karung’o Kamau, raia hao wa Tanzania  wameripotiwa kufanya kazi bila leseni wamehojiwa na wako chini ya uchunguzi wa mamlaka ya usalama nchini Kenya.

“Katika wiki moja iliyopita tumewakamata na kuwaweka chini ya ulinzi Watanzania 23 kwa kushiriki uvuvi katika bahari ya Hindi upande wa Kenya kinyume cha sheria. Walipelekwa mahakamani, na baadaye wakatolewa mara baada ya kupata dhamana,” – Kamau.

Kamau pia alibainisha kwamba wavuvi kutoka Tanzania na visiwani Pemba wamekuwa wakivua kinyume cha sheria kwa gharama za wenyeji.


Post a Comment

Previous Post Next Post