Vinara wa ligi kuu nchini, Simba imefanya maamuzi magumu baada ya kumtema mshambuliaji wake raia wa Burundi, Laudit Mavugo kwa ajili ya kuongeza makali mengine kwenye safu yao ya ushambuliaji.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inaeleza, Mavugo tayari amepewa taarifa ya kutemwa kwake na nafasi yake inatarajiwa kuzibwa na mshambuliaji raia wa Msumbiji Antonio Domingues.
Aidha, Simba inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa tayari imemalizana na nahodha wake, Method Mwanjali ambaye inaelezwa nafasi yake itazibwa na beki ‘kisiki’ wa Lipuli raia wa Ghana, Asante Kwasi.
Simba inatajwa kuwa tayari imemalizana na beki huyo na muda wowote atasaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.
“Huyo mshambuliaji kutoka Msumbiji hana shida, na kila kitu kinaenda sawa, kwa Kwasi kuna baadhi ya mambo yanakamilishwa kwa pande zote Simba na Lipuli na siku yoyote,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Pia Simba ipo mbioni kumpa mkataba mshambuliaji Jonas Sakuwaha ambaye atachukua nafasi ya Mghana Nicolaus Gyan ambaye ameshindwa kuonyesha makali yake kwenye kikosi hicho cha Kocha Joseph Omog.
Mavugo na Gyan walipewa nafasi kubwa ya kuwika kwenye kikosi hicho lakini mambo yameenda tofauti na kulazimika viongozi wa Simba kufanya maamuzi ya kuwatema.
Wakati upande wa Simba mambo yakiwa hivyo, watani zao Yanga wenyewe wametumia dirisha dogo la usajili kwa kuongeza wachezaji wawili tu.
Yanga imemsajili nyota wa Serengeti Boys, Yohana Nkomolwa pamoja na beki raia wa Kongo Fiston Kayembe kutoka Balende FC ya nchini kwao.
Kwa upande wao, Azam FC wenyewe wamemsajili mshambuliaji kutoka klabu ya Liberty Professional ya Ghana, Bernard Arthur ambaye anachukua nafasi ya Mghana mwenzake Yahya Mohammed aliyeachwa.
Aidha nyota wa Mbeya City aliyewahi kutamba na klabu za Yanga, Simba na Azam FC, Mrisho Ngasa, ameachana na timu hiyo na kujiunga na Ndanda FC
ULIIKOSA HII..? MSIKIE MZEE WA YPAKO ANACHO SEMA KUHUSU PESA

Tags
Michezo