REFA AOMBA RADHI BAADA YA KUMPA MCHEZAJI KADI YA NJANO

Beki wa Bournemouth Adam Smith amesema mwamuzi Jon Moss alimuomba radhi baada yake kumuadhibu kimakosa wakati wa mechi.

Moss alimuonesha kadi ya manjano bada ya kumpa mkwaju wa penalti baada yake kuanguka alipokabwa na beki wa Southampton wakati wa mechi ambayo ilimalizika sare ya 1-1 Jumapili.

Mechi ikiwa dakika ya 32, na mabao yakiwa 0-0, Smith alianguka baada ya kukabwa na Sofiane Boufal.

Badala ya kupewa penalti, Moss alimlisha Smith kadi ya manjano ya tano msimu huu.

Hii ina maana kwamba atakosa mechi yao ijayo.


"Kwa mwamuzi kunionesha kadi hilo halinisaidii kwa sababu ilikuwa kadi yangu ya tano ya manjano msimu huu," amesema Smith.

"Nilizungumza naye baadaye na akaniomba radhi, na akasema ilifaa kuwa penalti.

"Sina tatizo kwamba alikiri makosa lakini Hali kwamba aliniadhibu na hilo haliwezi kubadilishwa ina maana kwamba sitaruhusiwa kucheza mechi ijayo".

Meneja Eddie Howe amesema hajui refa alikuwa ameona nini "lakini hiyo ndiyo soka."



Bournemouth watakutana na Crystal Palace ugenini Jumamosi Southampton nao wawe wenyeji wa Arsenal Jumapili.

Bournemouth watakutana na Manchester United, Liverpool na Manchester City mechi zao zijazo nyumbani, katika unaoonekana kuwa msururu wa mechi ngumu kwao.


Post a Comment

Previous Post Next Post