MKUU WA GEREZA ATOA TAARIFA KUHUSU BABU SEYA



Dar es Salaam. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mboje amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha taratibu za kumtoa gerezani Nguza Viking na mwanaye Papii Kocha.

Mboje amesema hayo baada ya Rais John Magufuli kuwasamehe wafungwa hao ikiwa ni miaka 56 ya uhuru wa Tanzania.

Akizungumza na SWAHIBA BLOG leo Jumamosi jioni, Mboje amesema sasa hivi wanajaza fomu na itakapofika saa  11 watawaachia wafungwa hao.

Tarari ndugu jamaa na marafiki wa wanamuziki hao wako nje ya gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam wakiwasubiria.

Ndugu hao ambao wameonekana wakiwa kwenye magari huku wengine wakizunguka zunguka nje ya gereza hilo kusubiria taratibu za wanamuziki hao kukamilika ili waachiwe.




Post a Comment

Previous Post Next Post