MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA ATANGAZA KUJITOA KWENYE UCHAGUZI

Dar es Salaam. David Djumbe
aliyeteuliwa jana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea ubunge Singida Kaskazini kupitia Chadema amejitoa rasmi.

Djumbe amewasilisha  leo Desemba 20, 2017 kiapo cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida na barua ya adhima yake hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Singida, Rashid Mandoa.

Akizungumza na Mwananchi amesema ‘’ni kweli nimejitoa na nimekwisha kuwasilisha barua na kiapo cha mahakama kwa msimamizi wa uchaguzi.”

Katika barua ya DJumbe ya Desemba 19, 2017 kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi amesema ‘’…kwa hiari yangu mwenyewe si kushawishiwa na mtu yoyote. Kwa hiari yangu nimeamua kujitoa kugombea nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chadema.”

Mbali na barua hiyo, Djumbe amewasilisha kiapo cha Mahamaka ya mwanzo ya Singida kilichosainiwa na Kamishna wa kiapo Flora Ndale cha Desemba 20, 2017 kinachoeleza dhamira kuu ni kujitoa kushiriki uchaguzi huo.

Katika kiapo hicho ambacho Mwananchi imepata nakala yake kinaoneshwa kimepokelewa na msimamizi wa uchaguzi wa Singida Kaskazini na kugonga mhuri na saini.

Hata hivyo, Mwananchi lilipomtafuta Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mandoa amesema bado taratibu zinaendelea na atatoa taarifa baadaye juu ya suala hilo.


Post a Comment

Previous Post Next Post