Yadaiwa mganga wa jadi alitaka wafanye vitendo hivyo ili kujilinda na risasi kutoka kwa maadui
Kinshasa, DRC. Mahakama ya kijeshi katika Jimbo la Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imehukumu maisha jela mbunge Fréderic Batumike na watu wengine 11 kwa kosa la kuwabaka watoto mashariki mwa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na mtoto wa mwaka mmoja.
Awali, mbunge huyo aliomba kuongezwa majaji wengine wawili, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na mahakama na kufanya kesi hiyo kuendelea kusikilizwa.
Hukumu hiyo imekaribishwa kwa mikono miwili na wengi huku pia ikiungwa mkono na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Awali watuhumiwa hao walidaiwa kufanya vitendo hivyo baada ya kuambiwa na mganga mmoja wa jadi kuwa ingekuwa kinga dhidi ya risasi kutoka kwa maadui.
Wanaharakati wa haki za binadamu wanauona kwamba kesi hiyo ni muhimu na ina uzito mkubwa katika harakati za kukabiliana na hali ya kutowaadhibu wa husika wa matukio mbalimbali ya ubakaji.
Taarifa iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Physicians for Human Rights, ilisema kuwa kwa muda mrefu wabakaji nchini Kongo wamekuwa wakijiona kama wasioweza kuwajibishwa kisheria na kuongeza kwamba polepole, taswira hiyo imeanza kubadilika.
Washukiwa waliaminika kuwa wanamgambo wa kundi linalojiita “Jeshi ya Yesu,” wakiongozwa na mbunge Batumike.
Mahakama hiyo aidha iliamuru kila muathiriwa alipwe fidia ya Dola za Marekani 5,000 na 15,000 kwa familia ambazo jamaa zao waliuawa kwa kupinga au kushutumu vitendo vya waasi.
Shirika hilo lilisema hii ni mara ya kwanza kwa ofisa anyehudumu serikalini kupatikana na hatia ya kuwajibika kwa vitendo vya uhalifu uliotekelezwa na waasi ambao aliwadhibiti na kuwafadhili.
Ripoti zinasema zaidi ya wasichana 40 wamebakwa nchini humo. Msemaji wa muungano wa mawakili wa upande wa utetezi wakili Charles Kubaka Sikura amesema licha ya kesi hiyo kuanza kwa kuchelewa lakini wameridhiwa na hatua hiyo.
Wakati huohuo mawakili wa mbunge huyo wamekosoa namna kesi hiyo ilivyoendeshwa, wakisema majaji wamekua wakishinikizwa na baadhi ya vigogo serikalini kuchukua hatua kali dhidi ya mteja wao.
Wamepanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Kwa upande wa raia wameomba mali ya mbunge huyo wapewe waathirika wa matukio ya ubakaji ili waweze kujimudu kimaisha.

Tags
Kimataifa