CCM YAPATA PIGO WILAYA YA MISUNGWI

Diwani wa Kata ya Kanyelele wilayani Misungwi, Paschali Kilangi (46) amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa malaria.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Fredirick Nyoka amesema diwani huyo aliugua wiki mbili zilizopita ambapo ndugu walilazimika kumsafirisha kwenda hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya matatibu hadi umauti ulipomkuta.

“Tumepokea kwa masikitiko kifo cha diwani huyo kwa sababu alikuwa mchapakazi na mwadilifu, utendaji wake utadumu milele kwa wakazi wa kata ya Kanyelele na halmashauri kwa ujumla,” amesema Nyoka

Ofisa  habari wa halamashauri hiyo, Thomas Lutego amesema  halmashauri hiyo ina jumla ya madiwani 37 ambao wanajumuisha wakuteuliwa na mbunge.

Amesema kifo cha diwani huyo kimetokea ikiwa ni miezi sita tu tangu diwani mwingine wa Kata ya Kijima kufariki dunia.

Post a Comment

Previous Post Next Post