
Baraza kuu la kiislam Nchini (BAKWATA) leo limempokea Mwanazuoni wa Kiislam Mkubwa wa kidunia Abib Omar Bin Hatith kuto inchin Yemen kwa ziara ya Siku mbili
Akizungumzia ujio wa mwanazuoni huyo, Mufti Mkuu wa Tanzania sheikh Abubakary Zubery amesema kuwa amekuja pamoja na mambo mengine ataombea nchi yetu iwe na amani na upendo
" Mwanazuoni huyo tulimwomba aje kwa zaidi ya miaka miwili na tunashukuru amekubali ombi letu amekuja sasa tuko tayari kupokea aliyotuletea"' Amesema Sheik Abubakary.
Rais Mstaafu Alhaji Hassan Mwinyi amesema kuwa ujio wa Mwanazuon huyo ni ishara kuwa nchi yetu ina amani na upendo maana anahitajiwa na nchi nyingi.
Mwanazuoni- Abib Omar bin Hatith |
Imam wa Mskiti wa Shibu ulioko Mobasa nchini Kenya amesema kwa wako tayari kupokea yale atakayowapa
"Sisi tumejiandaa kupokea yale aliotupa mwanazuoni huyu wa kidunia.
Tags
dini