KAFULILA KACHUKUWA KADI CCM

Admin
By -
0


Dar es Salaam. Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-15 kwa tiketi ya Nccr-Mageuzi, David Kafulila amejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya kujivua uanachama Chadema hivi karibuni .

Novemba 22, Kafulila aliyepata umaarufu baada ya kuibua sakata ufisadi wa Escrow, alitangaza kujiengua Chadema akidai vyama vya upinzani havina dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi na kwamba muda ukifika atatangaza anakokwenda.

Lakini leo, Ijumaa Novemba 24, 2017, Kafulila ameibukia kwenye  mkutano wa kampeni wa  CCM Kata ya Mbweni na kutangaza kujiunga na CCM alipoitwa jukwaani na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Hamphrey Polepole.

Baada ya kuwasili katika eneo hilo kisha kupanda jukwaani Kafulila akiwa amevaa kofia ya rangi ya kijani alishangiliwa na wafuasi na wanachama wa CCM huku wengi wakisikika wakisema David Kafulila atua CCM.

Akizungumza na wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano huo, Kafulila amesema ; “ Nashukuru Katibu wa Itikadi na Uenezi (Polepole), mwenyeikiti wa wilaya, wajumbe wa Nec, mwenyekiti wa vijana wa Taifa na wabunge akiwamo Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe,”amesema Kafulila.

 Hatua hiyo ya Kafulila ilimshangaza mkewe Jesca Kishoa aliyemtaja mumewe huyo kuwa ni mtu aliye kundi la wanasiasa wasio na msimamo.

Kishoa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mkoa wa Singida amesema mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangaa kaingia katika mtego mbovu.

“Bado naamini Chadema ni mahali sahihi kabisa ambako siwezi kufikiri siku moja nitatoka, hivyo siyumbuki kwa hilo na wanaonipigia simu watambue hilo,” alisema Kishoa jana katika mkutano wake na wanahabari Dodoma

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)