JINSI YA KULINDA SIMU AU KOMPUTA YAKO ISIPATE VIRUS

Admin
By -
0
Virus katika computer/simu ni nini?
Hii ni programu inayojiingiza katika mfumo wa computer bila idhini ya mtumiaji wa computer na kuathiri utendaji kazi wa computer. Husambaa kutoka katika computer moja kwenda nyingine kwa kupitia njia za vifaa vya computer vigumu vyenye kutunza kumbukumbu(storage devices) na pia kwa njia ya mtandao. Virus hujifanya kuwa mfano wa file kama picha, audio, video na programu nyingine. Vifaa vilivyounganishwa na internet viko katika mazingira hatarishi zaidi ya kupata virus.

Virus katika computer husababisha kutetereka katika ufanyaji kazi wa computer hiyo. Hata hivyo kabla ya kuendelea ningependa tuone dalili za virus katika computer:

Dalili za virus katika simu/computer
*Ni ngumu kutambua haraka kama tatizo husika limesababishwa na virus au kuna matatizo katika vifaa vilivyounganishwa katika computer yako (Hardware).

Computer inaanza kuwa na tabia za ajabu ambazo haujazoea kuziona kwa mfano inazimika ghafla na kuwaka.Unaona meseji au picha usizozitegemea.Unasikia milio isiyo na mpangilio bila kufahamu chanzo chake.Programu zinajifungua tu bila wewe kuzifungua.Computer inaganda/inasimama tuli mara kwa mara na programu zinafunguka polepole kupita kiasi.Meseji zenye Errors zinakuwa nyingi.Unagundua kuwa mafaili yamefutikaIcon au picha za mafolder zinakuwa na ukungu (Blur)Web Browser yako kama Mozilla Firefox au Google Chrome inakuwa na tabia zisizo za kawaida kwa mfano ukiifunga haifungiki.

Hizo ni dalili tu baadhi, TAMBUA kwamba sio lazima matatizo hayo yasabishwe na virus huweza kuwa na chanzo kingine cha kawaida kwa mfano kama RAM yako ni ndogo na umefungua programu nzito lazima zichelewe kufunguka.


Ufanye nini sasa?

Kwanza usi panic! Computer nyingi katika hali ya kawaida huwa na tatizo mojawapo kati ya hayo niliyoyataja hapo juu. Internet kama nilivyosema hapo awali ni adui mkubwa katika afya ya computer, lakini hatuna jinsi kwa sababu internet ni lazima tuitumie. Baada ya hapo unaweza kufanya yafuatayo:

Chomoa au katisha mawasiliano ya internet na computer yako. Chomoa modem au wi-fi au cable. Pia katika simu unaweza kuzuia internet connectivity.Hakikisha kwamba Antivirus yako iko updated hii ni MUHIMU sana ku update antivirus yako. Hata hivyo kama unahisi computer yako ina virus ninakushauri kwanza utafute antivirus ambayo iko updated kutoka kwa rafiki yako au kutoka katika computer nyingine kisha Uninstall ya kwako na install hiyo mpya kisha SCAN computer nzima.Ukiona programu inajifungua na kisha kukuonesha ujumbe ikikuonya kuhusu computer yako kuwa na Virus au Spyware usibonyeze kitu chochote ndani yake badala yake bofya ALT+F4 ili uikate bila kuibonyeza.Pia usipende kubonyeza bonyeza matangazo unayoyaona katika internet hasa yale yanayojifungua yenyewe,mengi huwa na virus.Usipende kufungua flash au memmory card ambazo hauziamini katika computer yako pia usichomeke memmory card au flash disk yako katika computer ambayo hauamini usala wake

Uzuri wa virus ya computer ni kwamba inaweza kutibika kirahisi (Hasa virus za kawaida kama Autorun na Shortcuts). Zipo programu nyingi za kutibu virus. Hata hivyo Anti virus inabidi ui Update angalau kila siku au baada ya siku chache kwani virus zinatengenezwa kila siku hivyo inabidi antivirus yako iwe ya kisasa kila siku. Anti virus hizi huuzwa kwa bei ghali. Lakini zipo za bure pia.


Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)