Wakulima wa mahindi katika wilaya ya Serengeti, mkoani Mara wamelazimika kutumia Mkojo wa na majivu ili kudhiti funza na wanaoharibu mahindi shabani.
wamesema kuwa wanatumia mkojo na majivu kutokana na dawa za madukani kuwa na gharama za juu.
Mkazi wa Kijiji cha Ringw'ni Bw. Ryoba Marwa mmoja wa wakulima hao amesema kuwa wanachukua mkojo wa binadam na kuchanganya na majivu baadaye humwagilia kwenye mahandi shambani.
"Mkojo wa binadam unaonekana kuua wadudu shamabani, ila changamoto ni kuupata wa kutosha kwa sababu huwezi kwenda kuomba kwa jiran, watadhani unaenda kufanya mambo a kishirikina" amesema bw. Marwa.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wilaya ya Serengeti Bw. Simon Warioba amesema kuwa funza hao wanaoshambulia mahindi ni hatari sana.
"Hawa funza ni hatari saana serikali haina dawa ya kuwaua, na hata hawa wanaotumia njia za asili wanaua funza tu ila mayai anabaki yakiwa salama hivyo kuzaliana tena," Amesema Warioba
Afisa huyo wa Kilimo amefafanua kuwa wanajitahidi kutoa ushauri kwa wakulima hao waweze kununua dawa za madukani ili kuwaangamiza kabisa jamii ya wadudu hao.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Serengeti Bw. Juma Porini amewataka wataalam wa kilimo kwenda vijijini kuwasaidia wakulima kuwaangamiza wadudu hao kwa wasipofanya hivo wilaya itakumbwa na janga la njaa.