Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe |
Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amezitaka Jumuia ya Afrika Mashari (EAC) na Benki ya Dunia (WB) kufanya uchunguzi kubaini kama Takwimu za pato la Taifa kwa robo ya Pili ya mwaka 2017 au ni za uongo.“Jumuia ya Afrika Mashariki na Benki ya Dunia wafana uchunguzi kuhusu takwimu hizi kama “zimepikwa” ili hatua za kisheria zichukuliwe”. Amesema hayo mbele ya waandishi wa jana habari jiji Dar es Salaam.Bw. Zitto amenilinganisha takwimu za uchumi zilotolewa na Benki Kuu (BoT) kuwa zinafanana na za miaka mine iliopita.“Hizi Takwimu zimepikwa kuonesha uchumi umekua wakati ukweli uchumi umeshuka” amesema Zitto
Zitto ambae pia ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa serikali inapaswa kuangalia upya sera ya fedha ili ziwe zinabaki nchini kuliko kutoka nje ya nchi.
“Serikali ya awamu ya Tano imejitahidi kuziba mianya ya ukwepaji kodi lakini tunashudia uchumi ukishuka”Amesisitiza Zitto.
Amependekeza kuwa Mchaguzi and Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) kuchunguza mapato yaliyo kusanywa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuanzia Julai na Agosti mwaka huu na majibu yake yawekwa wazi.
Wiki iliopita Mbunge huo alitoa madai kama haya kuwa takwimu ya uchumi kukua “zimepikwa” taofauti na Uhalisia.
Tags
Kitaifa