
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Andrew Massawe jana aliitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mamlaka hiyo kuwa ni Dodoma, Mbeya, Njombe, Songwe, Singida, Simiyu, Geita, Mwanza, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Iringa.
Mamlaka hiyo pia kesho inatarajia kuzindua usajili wa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho hivyo mkoani Mtwara. Alisema wanashirikiana na Wakala wa Ufilisi, Usajili na Udhamini (RITA), Idara ya Uhamiaji na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuhakikisha kila mwananchi anayepatiwa kitambulisho amekidhi sifa ya uraia wake.
Mfano(Sample) wa Kitmbulisho cha Taifa |
Alisema baada ya kukamilisha utambuzi, taarifa zote zilizokusanywa katika mikoa hiyo 12, zitawasilishwa makao makuu Dar es Salaam kutolewa vitambulisho na mamlaka hiyo itatoa namba za utambulisho kwa wananchi waliopitia michakato yote
Bw. Massawe ailiongeza kuwa hadi kufikia Juni mwakani, wananchi wote waliopo nchini wenye sifa na wanaostahili kupatiwa vitambulisho hivyo vya taifa watakuwa wameshapatiwa namba ya utambulisho na ifikapo Desemba mwaka huo, watakuwa wamepata vitambulisho.
Mkurugenzi huyo alisema, kutolewa kwa vitambulisho hivyo ni utaratibu endelevu kwa kuwa kila mwananchi aliyefikisha umri wa miaka 18 atapata kitambulisho hicho. Alitaja vitu ambavyo mtu anatakiwa awe navyo kukidhi vigezo vya vitambulisho hivyo kuwa ni kuwa na cheti cha kuzaliwa na endapo hana cheti hicho ni lazima uhamiaji imthibitishe, cheti cha kitaaluma, kadi ya kupigia kura au hati ya kusafiria.
Tags
Kitaifa