Rais John Pombe Magufuli |
Mawakili hao walikuwa miongoni mwa watu 13 waliokamatwa katika hoteli moja mjini Dar es Salaam .
Mapema mwaka huu, serikali ilipiga marufuku baadhi ya kliniki binafsi kutotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikisema zilikuwa zikukuza mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini Tanzania.
Hatahivyo, Sibongile Ndashe anasema kuwa walikuwa hawana haki ya kuwakamata na ameishtumu mamlaka ya Dar es Salaam kwa kuwakamata yeye na wenzake.
Bi Ndashe anasema kuwa hatua yao ya kutaka kujua sababu za wao kutimuliwa nchini humo hazikuangaziwa.
Kamanda Polisi kanda Malaam ya Dar es Salaam aliwaambia wanahabari kuwa kabla ya mawakili hao kukamatwa kwamba walikuwa wakikuza mapenzi ya jinsia moja.
Kukamatwa kwao kunajiri kufuatia hotuba ya mwezi Septemba iliotolewa na aliyekuwa naibu waziri wa afya Dk. Hamis Kingwangala ambaye aliapa mbele ya bunge kukabiliana na makundi yoyote yanayounga mkono wapenzi wa jinsia moja nchini humo.
Shirika la haki za kibinaadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kundi hilo linaweza kuishtaki serikali ya Tanzania kwa kupiga marufuku vituo vya afya vinavyowauguza wato waliopo katika hatari ya kuambukizwa ukimwi mbali na uagizaji wa kifaa cha mafuta ambayo yanaweza kutumika kujilinda dhidi ya HIV.
Tags
Kitaifa