Maisha ya mliliki wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited, (IPTL) Bilionea Harbinder Sethi yako hatarini kutokana na puto alilowekewa kuisha muda wake mahakama imeelezwa.
Wakili wa Sethi, Alex Balomi alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mshitakiwa huyo alipelekwa kufanyiwa vipimo Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini hadi leo hajapatiwa majibu yake ya vipimo wala kupatiwa matibabu.
Mbali na Sethi,
mshitakiwa mwingine ni James Rugemarila ambao kwa pamoja wanakabiliwa na
mashitaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababisha serikali
hasara ya m
mabilion ya shilingi.
Wakili Bomani alidai kuwa mshitakiwa huyo, ana puto tumboni ambalo limeisha muda wake, hivyo linapaswa kubadilishwa mwishoni mwa mwezi huu.
“Lengo la Mahakama hii kutoa amri ya kumpeleka mshitakiwa kupata matibabu lakini hakupata majibu ya vipimo ambazo ni taarifa zake binafsi" alisem wakili.
Mteja wetu ana wasiwasi kwa kuwa hajapewa majibu ya vipimo alivyochukuliwa kwa sababu ya athari ya puto lililowekwa tumboni,” alidai Balomi. Aidha, waliomba upelelezi wa kesi hiyo ukamilike kwani upande wa mashitaka unaonekana unazembea wakati watuhumiwa wanateseka gerezani bila sababu.
Akijibu hoja hizo, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai alidai kuwa Sethi alipelekwa hospitali Oktoba 13, mwaka huu na kwamba alipokea matibabu kutokana na vipimo vya daktari. Swai alidai suala la vipimo ni siri kati ya mshitakiwa na daktari, hivyo hayapaswi kuongelewa mahakamani.
Kesi hiyo itatajwa itwasilikizwa tena Novemba 10, mwaka huu, huku upanda wa utetezi ukita upandwa wa mashtaka ufanye uchunguzi haraka dhidi ya mteje wao.
Tags
mahamani