Akiongea katika ndahalo wa wagombea urais nchini Uganda, mgombea wa Chama cha The Democratic Alliance (TDA), Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi amesema kuwa kwa sasa Uganda inahitaji Rais kama Dk. John Pombe Magufuli wa Tanzania.
Alipopewa muda wa kueleza maneno yake ya mwisho katika mdahalo huo uliofanyika usiku wa Jumamosi na kuhudhuriwa na wagombea nane, Amama Mbabazi alisema “Sio suala la upinzani kushika madaraka bali ni kuhusu kumpata mtu sahihi kwa ajili ya Uganda mpya. Tuna bahati kuwa hapa nchi jirani na sisi kuna mtu anaitwa JPM, yaani John Pombe Magufuli wa Tanzania.
Hivi sasa Uganda inahitaji mtu kama Magufuli ambaye ameonyesha wazi kwa matendo kuwa ataipeleka mbali Tanzania,Ni Rais anaonekana mzalendo sana.
Huku Rais anauyemaliza muda wake, Yoweri Museveni akisikiliza kwa makini, Mbabazi alisema “Sielewi ni kwanini Waganda tunakuwa wazito kujifunza kutoka madarakani. Ni lazima tufanye mabadiliko ili tuachane na mawazo mgando.”
Post a Comment
0Comments
3/related/default