Hali ya Joni Woka bado ni tete,kaka yake aomba watanzania wamwombee.

Unknown
By -
0
Hali ya afya ya rapper Joni Woka ambaye siku mbili zilizopita alipata ajali ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso wakati anatengeza gari mitaa ya Sinza bado ni tete.
Kaka wa rapper huyo ambaye aliwahi kutamba kwa staili yake ya kurap kama mlevi amesema kuwa hali ya Joni bado sio nzuri na kwa sasa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuchomwa na kitu hicho kilichotoka kwenye mtungi wa gesi ya Ac.
kitu hicho kilichomchoma kimeingia kama inch 3,kwa hiyo damu ikawa imemwagikia kwa wingi ndani ya kichwa kwa hiyo ndio tatizo lake kubwa,hali yake ngumu sana yuko ICU toka juzi alivyoingia hajaamka” alifunguka ndugu wa Joni Woka aliyejitambulisha kwa jina la Omari na kuwaomba watanzania wamwombee dua.
Source: Clouds
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)