CHELSEA YAMPA IBRAHIMOVIC REKODI MPYA KWENYE SOKA

Unknown
By -
0
Usiku wa February 16 ulikuwa ni wa Ulaya (UEFA Champions League) ambap[o ilipigwa michezo miwili ya hatua ya mtoano (16 bora). PSG ilikuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Parc des Princes kuikabili Chelsea huku Benfica nayo ikiwa kwenye dimba la Estádio da Luz kupambana na Zenit St Petersburg
Mchezo uliopewa uzito wa juu ni wa PSG vs Chelsea kutokana na uhasimu ambao umekuwepo kati ya timu hizo mbili ambazo jana zilikuwa zikikutana kwa mara ya 16 kwenye ligi ya mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa PSG kuichapa Chelsea kwa bao 2-1, mchezaji Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la kwanza kwenye mchezo huo na kuandika rekodi mpya kwenye maisha yake ya soka.
Superstar huyo wa Sweeden aliipatia PSG bao la kuongoza dakika ya 39 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo huo wa kwanza wa mtoano hatua ya 16 bora.
Ibra ilipacika mpira kwenye nyavu za Chelsea baada ya free-kick yake kumgonga John Obi Mikel na kutinga wavuni huku golikipa Thibaut Courtois akipotea vibaya na kushindwa kuuokoa.
Baada ya kupachika bao dhidi ya Chelsea, Ibrahimovic amefikisha mabao 46 kwenye michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Lakini kiamini usiamini, goli la usiku wa jana lilikuwa ni goli lake pekee kufunga kwa mpira wa adhabu ndogo (free-kick) kati ya magoli yote 46.
Goli la Ibra limemfanya aingie kwenye rekodi ya wafungani bora wa muda wote wa Champions League pamoja na European Cup akilingana magoli na wakali kama mkongwe wa Ureno Eusebio, Karim Benzema na Filippo Inzaghi lakini wote hao wanatofautishwa na mechi walizocheza huku Ibra akiwa ameheza mechi nyingi zaidi kuliko wengine (116) .
Lakini pia, Zlatan Ibrahimovic amefunga kwenye mechi tatu za mwisho mfululizo za Champions League wakati huohuo amehusika kwenye kupatikana kwa magoli tisa kwenye mechi 11 za mwisho ilizocheza PSG kwenye mashindano yote. (magoli 7, assists 2)
Matokeo ya mchezo kati ya Benfica vs Zenit St Petersburg
Kwenye mchezo kati ya Benfica vs Zenit, Benfica walifanikiwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zenit St Petersburg.
Video ya magoli yote ya mechi ya PSG vs Chelsea

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)