YANGA NA AZAM ZASHINDWA KUTAMBIANA TAIFA

Yanga washindwa kitambia azam f.c taifa leo baada ya dolnad ngoma kuishindia yanga goli la kwanza katika kipindi cha kwanza

goli lililowafanya yanga kwenda mapunziko wakiwa mbele kwa goli 1-0 dhidi ya Azam F.C

Kipindi cha pili Azam walirejea kwa kasi wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara huku wakimiliki mpira kwa dakika za katikati ya kipindi cha pili wakati Yanga kwa upande wao walikuwa wakicheza mipira mirefu na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

kipre Tchetche aliyeingia kipindi cha pili kuchua nafasi ya Alan Wanga aliifungia Azam goli la kusawazisha dakika ya 83 akiunganisha pasi ya Farid Musa na kuufanya mchezo kuwa sare kwa goli 1-1.

Wakati dakika zikiwa zimeyoyoma, Yanga walipata penati baada ya golikipa wa Azam Aishi Manula kumwangusha mchezaji wa Yanga Simon Msuva kwenye eneo la hatari lakini Manula alipangua penati hiyo iliyopigwa na Thabani Kamusoko.

Post a Comment

Previous Post Next Post