Lowassa Azuwa Balaa MBEYA

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Liberatus Mwang'ombe
Lowassa agombanisha wafuasi wa CUF na CHADEMA Mbarali Mbeya. Wafuasi hao walikuwa wakimsubiri mgombea urais anayewakilisha UKAWA kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa, chanzo cha ugomvi ni hiki, wafuasi wa Chadema wasema hawamtambui mgombea wa CUF ambaye (UKAWA) walipendekeza jimbo hilo wagombee CUF, lakini CHADEMA waliamua kumsimamisha mgombea wao na kukiuka makubaliano ya UKAWA. Katika vurugu hizo iliwalazimu Polisi watumie mabomu ya machozi kutuliza ghasia hizo, hata hivyo waliozidiwa nguvu na kuomba msaada wa Askari Magereza kusaidia kutuliza vurugu hizo.

Jimbo hilo limekuwa katika mvutano wa muda mrefu kati ya CHADEMA na CUF. Vile vile jimbo hilo lina ushindani mkubwa katika kinyang'anyiro cha ubunge baina ya CCM, CHADEMA na ACT ambapo ACT wamemsimisha Kilufi aliyekuwa mbunge wa zamani kwa tiketi ya CCM ambaye alijivua uanachama baada ya kushindwa kwenye kura za maoni na kuhamia CHADEMA ambapo uanachama wake ulidumu kwa siku 7 baada ya kuona amekosa nafasi ya kugombea ubunge akahama tena na kujiunga na ACT ambapo alipata nafasi hiyo ya kugombea ubunge.

Post a Comment

Previous Post Next Post