
Mwanasisa maarufu wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jean pierre Bembe amerejea rasmi nyumbani baada ya kukaa miezi kumi ugenini.
Bemba alirudi Congo hapo jana kutoka Brussels Ubelgiji katika ndege ya kibinafsi na kupokewa na umati wa watu waliokusanyika Kinshasa kumlaki.
Washirika wake Bemba anasema amerudi rasmi nchini kutoa usaidizi kwa mpinzani Martin Fayulu ambaye anasisitiza kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Ni ziara ya pili ya mwanasisia huyo nchini DRC baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC baada ya kutumikia kifungo cha miaka kumi gerezani.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa Mbelechi Msochi anasema alihotubia kwa mara ya kwanza umati wa watu uliokusanyika na kueleza raia kile ambacho upinzani unadai ndio ukweli kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu huo,
'Mahakama ya katiba inapaswa kuimarisha demokrasi nchini mwetu, badala yake imekuwa kama saratani inayoharibu taasisi zetu. Mmeona jinsi bunge letu limekuwana watu ambao hawakuchaguliwa ndio wamelitawala... hiyo inachafua jina la nchi yetu ugenini. Sio viongozi tu walio na haki ya kujenga nyumba'.
Bemba anapanga kusalia nchini Congo kwa muda mrefu katika kuongoza mfululizo wa maandamano aliyopanga kwa lengo la kudai haki ya uchaguzi huo.
Bemba alirudi Congo kuonesha azma ya kutaka kugombea katika uchaguzi wa mwaka jana lakini ombi lake lilitupiliwa mbali na tume huru ya uchaguzi ya DRC.
Alirudi Ubelgiji na kutangaza kuungana na Moise katumbi mgombea mwingine wa upinzani, pamoja na M
artin Fayulu kupitia muunganowa Lamuka.

Umati uliokusanyika mara hii ni mdogo ukilinganishwana uliokuwepo wakati Bemba aliporudi Congo kwa mara ya kwanza kutoka uhamishoni mnamo Agosti mwaka jana baada ya kuishi kwa zaidi ya muongo mmoja nje ya nchi hiyo.
Kiongozi mwenza wa upinzani Moise Katumbi alirudi kutoka uhamishoni mwezi mmoja uliopita.
Bemba aligombea urais dhidi ya rais Joseph Kabila mnamo 2006 na alishindwa.
Alikaa kwa miaka 10 katika mahakama ya ICC kwa uhalifu uliotekelezwa na wanajeshi wake katika Jamhuri ya Afrika ya kati kabla ya kuondoshewa mashtaka na hatimaye kuachiwa huru baada ya kukata rufaa.
Anarudi nchini Congo wakati rais Tshisekedi ameingia katika makubaliano ya serikali ya muungano na kiongozi aliyemtangulia Kabila, ambaye ana uwingi bungeni.

Mambo Makuu kumhusu Jean Pierre Bemba
Jean-Pierre Bemba alizaliwa mwaka 1962 kwenye mkoa wa kaskazinia magharibi wa Equateur, Baba yake, bilionea Bemba Saolona alikuwa rafiki wa karibu wa Mobutu Sese Seko.
Baba wa watoto watano amemuoa binti wa Mobutu na kusababisha kupewa jina "Mobutu Mdogo" kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na kiongozi huyo wa zamani wa DRC.
Novemba mwaka 1998 Bemba alibuni kundi la waasi MLC kwenye mkoa wake wa nyumbani wa Equateur.
Vikosi vyake baadaye vilihusika kwenye mzozo kati ya mwaka 2002 na 2003 kwenye nchi jirani ya DRC, vikipagana kwa ushirikiano na vikosi vilivyokuwa watiifu kwa aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ange-Felix Patasse, ambaye alikuwa akipingwa na aliyekuwa mkuu wake wa majeshi wakati huo Francois Bozize.
Agosti mwaka 1999, MLC ilisaini mkataba wa amani wa Lusaka ambao ulinuia kufikisha kikomo mapigano nchini DRC.
Aligeuza MLC kutoka kundi la waasi na kuwa chama cha kisiasa kufuatia kusainiwa makubaliano ya amani ya mwaka 2002.