hiki ndicho kilichomkuta tid

Admin
By -
0







MSANII wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’, jana aliposti picha kwenye ukarasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa na uvimbe na damu kwenye sehemu ya uso ambayo ilizua maswali mengi kwa watu.



Katika picha hiyo aliyoiweka mtandaoni, aliandikia ujumbe unaosema kuwa: “Washamba bwana wakiona tu unasikika wanaamua kukupiga hivi, inaumiza, jambazi anaweza kukufanya chochote sababu yeye jambazi na ana muonekano wa kijambazi.”




Championi Ijumaa lilimtafuta TID, ambapo alipopokea simu alishindwa kuzungumza juu ya mkasa huo uliomtokea huku akisema hawezi kueleza kwa kuwa yupo hospitalini na atazungumza pindi atakaporuhusiwa.



“Nipo hospitalini, siwezi kuzungumza vizuri kwa sasa lakini nikiruhusiwa nitaweka wazi kila kitu juu ya kile ambacho kimenikuta,” alisema TID.

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)