
Virusi vya ukimwi vikianza kushambulia mwili hujionyesha na
dalili kadhaa mwanzoni lakini pia dalili hizo huja kulingana na hatua nne kuu
ambazo shirika la afya duniani lilikaa na kuzipanga baada ya kufanya utafiti wa
mda mrefu..
Ugonjwa huu ambao unashambulia sana kinga ya mwili huja na
hatua na dalili zifuatazo kama ilivyotajwa.
HATUA YA KWANZA.[STAGE ONE]
Kuvimba kwa tezi zote za mwili.
HATUA YA PILI
Kupungua uzito chini ya asilimia kumi bila sababu maalumu.
Kuugua mara kwa mara magonjwa ya kifua
Fangasi za kwenye ngozi na kucha.
Mkanda wa jeshi
Kuwashwa sana ngozi
HATUA YA TATU
Kupungua uzito kwa
zaidi ya asilimia kumi bila sababu yeyote.
Kuharisha bila sababu zaidi ya mwezi mmoja..
Fangasi za mdomoni
Kifua kikuu.
Upungufu wa damu
Magonjwa ya mdomoni mfano gingivitis..
Homa za mara kwa mara.
HATUA YA NNE..
Kukonda sana ..
Fangasi za koo la chakula..
Kuchanganyikiwa kiakili.
Kansa ya ngozi mfano karposis sarcoma
Kupungua na kuharibika kwa uwezo wa mishipa ya fahamu..
Kuharisha zaidi na zaidi.
upofu wa macho
Kumbuka, mgonjwa akishahamia kwenye hatua Fulani harudi
nyuma ataendelea na hatua za mbele.
Moja ya vigezo vya mgonjwa kuanzishiwa dawa za kurefusha
maisha ni kufikia hatua ya tatu au ya nne, mgonjwa mjamzito na mtoto mdogo.
Watu wengi wakisoma makala kama hizi wanafikiri ukimwi ni
watu Fulani lakini naomba nikwambie msomaji ukimwi upo Na unaua…. japokua
ukifuata utaratibu wa matibabu utaishi maisha marefu na ya kawaida kama
wengine.
Hivyo unashauriwa kujizuia na ukimwi kama inavyotangazwa
kila siku, kupima mara kwa mara na kuanza matibabu haraka kama tayari umesha
athirika..kwa maelezo na ushauri zaidi soma hapa