Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imetoka sare tasa ya bila kufungana dhidi ya timu ya Mali katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Mataifa ya Afrika, Mchezo uliopigwa katika Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville nchini Gabon.