Mwanza mti wagoma kukatwa jua zaidi

"Leo Nimeshuhuhudia wananchi wa Pansiansi jijini Mwanza wakiwa wamefurika kuushuhudia mti unaodaiwa kuwa wa maajabu, eti ulikua unaondolewa kupisha ujenzi wa barabara iendayo airport."


Wanadai ETI ulipokua unakaribia kuondolewa na Grader Mti huo ukaongea na kusema.."Mniache hapa siendi kokote.." Mashuhuda wote waliofika hapo na kuwauliza, hakuna aliyethibitisha kuona kwa macho na kuthibitisha kwa sikio lake. 

Kila mtu alisikia tu taarifa hizo.... Wamejaribu eti kuukata na shoka utaongea.. wapiiii.. Kwa mujibu wa mashuhuda waliozuka mahala hapo wanadai mti huo una sauti ya kiume hivyo ni Babu na upo mwingine una sauti ya kike ambao ni Bibi.. 


Na kwamba eti Mti ulipokatwa ulitoa cheche na baadae ukatoa damu... dah .. "Nikacheka tu na kusema, kazi tunayo" Je wewe unaamini Nguvu za Giza?? 

Post a Comment

Previous Post Next Post